Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kutikisa katika mikoa mitatu ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma ndani ya siku nne, tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi, kesho uelekeo ni Songwe.
Agosti 28, 2025, CCM kilizindua kampeni zake Dar es Salaam, huku maelfu ya wananchi, wafuasi wa chama hicho wakijitokeza kwa wingi kusikiliza sera na Ilani ya chama hicho ili kufanya uamuzi sahihi Oktoba 29, 2025.
Baada ya uzinduzi huo, Samia alielekea Morogoro na kufanya mikutano katika wilaya zake na jana ilikuwa ni zamu ya Dodoma.
Baada ya kuhitimisha Dodoma, kesho anatajiwa kuendelea na kampeni hizo kwa upande wa Songwe.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED