Wastaafu wampigia debe Samia

By Romana Mallya , Nipashe
Published at 09:59 AM Sep 01 2025
Samia Suluhu Hassan
Picha: Mpigapicha Wetu
Samia Suluhu Hassan

Viongozi wastaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wampigia debe mgombea urais wa chama hicho, Samia Suluhu Hassan,kuwa ndiye dereva anayetosha kwenye nafasi hiyo, kwa kuwa ana leseni ya kimataifa.

Wastaafu hao ni Makamu Mwenyekiti mstaafu CCM,  Philip Mangula na Makamu Mwenyekiti mstaafu John Malecela.

Kauli hiyo wameitoa leo Agosti 31, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Tambukareli, Dodoma.

Makamu Mwenyekiti mstaafu CCM Mangula, amesema,”Ukiingia kwenye gari unatakiwa kuangakia leseni, na dereva wetu ana leseni ya kimataifa.Hao wengine mmh hatuwezi kufanya majaribio tunakwenda kwa hakika.”

Amesema yote anayosema yamepitishwa na ilani anayafahamu na anayaendeleza.

Makamu Mwenyekiti mstaafu CCM, Malecela amesema anamshukuru Rais Samia ambaye ameteuliwa kugombea urais CCM.

“Huko nyuma ukiangalia kwenye rekodi tangu Tanzania tuwe na uhuru wa kuchagua kiongozi wa nchi ambaye ni Rais, tuna mikoa miwili yenye rekodi nzuri Iringa na Dodoma.

“Mimi sina hotuba ya kutoa, nina jambo moja kuwaomba Dodoma rekodi za nyuma zinaonesha kwamba kila mara tunawapa marais kura nyingi, naomba safari hii wote Dodoma tutampe kura Samia.