Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeahidi kumaliza mchakato wa Katiba Mpya katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Kimesema kitahuisha mchakato wa Katiba Mpya, kitaendeleza pale ulipoishia na kuhakikisha inapatikana ndani ya miaka mitano ijayo.
Mgombea Mwenza wa Urais wa chama hicho, Dk. Emmanuel Nchimbi ametoa ahadi hiyo leo katika Uwanja wa CCM Dutwa mkoani Simiyu.
Pia, kimeahidi kuimarisha demokrasia na utawala bora nchini ili kila mwananchi aweze kushiriki katika shughuli za kijamii.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED