Rais Samia apatiwa tuzo kwa kuthamini wenye uhitaji

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:04 PM Sep 01 2025
news
Picha Mpigapicha Wetu
Waziri wa Ujenzi Abdalah Ulega akionyesha tuzo aliyoipokea kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan.Waziri wa Ujenzi Abdalah Ulega akionyesha tuzo aliyoipokea kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan.

WATOTO yatima kutoka katika vituo mbalimbali wametoa tuzo kwa watu ambao wamekuwa wakithamini maisha ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu ambako mmoja wa waliotunukiwa ni Rais Samia Suluhu Hassan.

Tuzo hiyo imetolewa leo Dar es Salaam wakati wa dua maalumu iliyoandaliwa kwaajili ya kumuombea kiongozi huyo wa taifa, na imepokelewa na Waziri wa Ujenzi Abdalah Ulega ambaye ni mgombea ubunge katika Jimbo la Mkuranga.

Watoto hao wamemuombea dua Rais Samia ya kumlinda katika safari yake ya kusaka kura wakati huu wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

1
Baada ya kupokea tuzo hiyo Waziri Ulega, amesema dua ya watoto hao ni njema kwa yeyote anayeombewa.

“Watoto ni vipenzi vya Allah. Hawa dunia yao inafika moja kwa moja kwa Mwenyezi Mungu. Niwapongeze sana kwa ubunifu huu, Mungu atamlinda rais dhidi ya ajali, magonjwa na mambo mengine,” amesema Ulega.

Pia Ulega amesema amevutiwa na ubunifu uliofanywa na waandaaji wa dua hiyo ambayo imefanyika katika wakati ambako kampeni za uchaguzi wa Oktoba 29 mwaka huu zimeanza kwa kasi kubwa.

2