Raila Odinga afariki dunia akitibiwa India

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 12:51 PM Oct 15 2025
Raila Odinga
Picha: Mtandao
Raila Odinga

Kiongozi wa Chama cha Orange Democratic Movement (ODM), Raila Amolo Odinga, amefariki dunia, akipatiwa matibabu nchini India.

Raila (80) amefariki leo, siku ya Jumatano, Oktoba 15, 2025, kwa mujibu wa baadhi ya vyombo vya habari huko nchini India.

Kifo cha Raila kimetokea siku chache baada ya kaka yake, Oburu Odinga, kufichua kuwa Raila alikuwa akipata matibabu nje ya nchi.

Oburu alibainisha kuwa hali ya Raila haikuwa mbaya sana na alikuwa anapona vizuri kabla ya kurejea nyumbani.

“Nataka niwaambie kwamba Raila yuko vizuri, kama binadamu mwingine yeyote alikuwa amechoka kidogo, na sasa anapumzika na kuendelea kuimarika; lakini hakuwa katika hali mbaya kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari,” amesema.

Vilevile, kabla ya kifo chake wiki iliyopita mitandao ilieneza taarifa kuhusu kifo chake, ingawa ulidaiwa ni uvumi na chama cha ODM.

CHANZO: The Hindu