Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ametembelea Makumbusho ya Rais wa Kwanza na Muasisi wa Taifa la Angola, Hayati António Agostinho Neto, katika eneo la Public Square, Jijini Luanda leo Aprili 08, 2025.
Katika ziara hiyo ya heshima, Rais Dk. Samia alipokelewa kwa heshima ya kijeshi kabla ya kuweka shada la maua kwenye Mnara wa Kumbukumbu wa Hayati Neto kama ishara ya heshima na ukumbusho kwa mchango wake mkubwa katika harakati za ukombozi wa Afrika.
Hayati António Agostinho Neto alikuwa kiongozi mashuhuri na mwanamapambano aliyesaidia sana katika kupigania uhuru wa Angola kutoka kwa utawala wa kikoloni wa Ureno. Uhusiano kati ya Tanzania na Angola umejengwa juu ya misingi ya mshikamano wa kihistoria na ushirikiano wa muda mrefu katika nyanja za siasa, uchumi na kijamii.
Ziara ya Rais Dkt. Samia nchini Angola inalenga kuimarisha zaidi ushirikiano wa kidiplomasia na kuongeza fursa za kiuchumi kati ya mataifa hayo mawili marafiki.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED