Rais Samia atengua uteuzi wa Polepole, aondolewa hadhi ya ubalozi

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 07:04 PM Aug 05 2025
Hamphrey Polepole
Picha: Mtandao
Hamphrey Polepole

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imethibitisha kuwa Rais Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi wa Hamphrey Polepole aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, na pia kumuondolea hadhi ya ubalozi.

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Dk. Samwel Shelukindo, kufuatia barua rasmi kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dk. Moses Kusiluka, ikieleza kuwa uamuzi huo umefanywa kwa mamlaka aliyopewa Rais chini ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma, Rais Samia amemuachisha kazi Hamphrey Polepole kwa msingi wa manufaa ya umma.

Uamuzi huo umeanza kutekelezwa rasmi kuanzia Julai 16, 2025.