MKUU wa Mkoa wa Morogoro Adam Kighoma Malima amesema mshindi wa maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki, atapatikana kutokana na bidhaa anazoonesha uwanjani na shamba darasa analoendeleza kwa wakulima eneo alikotoka.
Malima amesema hayo leo, wakati alipotembelea maonesho hayo yanayofanyika kwenye uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere, uliopo eneo la Tungi, nje kidogo ya manispaa ya Morogoro.
Amesema wakulima wameonekana kuitikia hasa katika upande wa mazao ya vipando na kutoa elimu kwa wakulima, jambo ambalo wanapaswa kulifanya kwa kuweka mashamba darasa kwenye maeneo wanakotoka, ili kuleta mageuzi yanayotakiwa kwenye kilimo nchini.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED