Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dk.Festo Dugange, amesema serikali imetumia Shilingi bilioni 107 kujenga vituo vya afya 367 nchini kati ya mwaka wa fedha 2020/21 hadi 2024/25.
Akijibu swali la Mbunge wa Kondoa Mjini (CCM), Ally Makoa, kuhusu upatikanaji wa fedha kwa ajili ya ujenzi wa majengo muhimu katika vituo vya afya vya Kondoa, Dk. Dugange alisema serikali inatambua changamoto zilizopo kwenye vituo vya Serya, Kolo na Kingale.
Amebainisha kuwa vituo hivyo vina upungufu wa miundombinu kama vile wodi za kulaza wagonjwa, jengo la mionzi, mortuary, sehemu za kufulia, njia za kutembelea wagonjwa na vyoo vya kuchomea taka.
Ameongeza kuwa ujenzi na ukamilishaji wa miundombinu hiyo utaendelea kufanyika kwa awamu kote nchini, ikiwa ni pamoja na vituo vya Kolo, Kingale na Mongoroma katika Halmashauri ya Mji wa Kondoa.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED