MAHAKAMA ya Mwanzo ya Mjini Morogoro, imewapandisha kizimbani vijana 14 wakazi wa mitaa ya Azimio na Mawasiliano, Kata ya Kihonda katika Manispaa ya Morogoro, wakikabiliwa na mashtaka tofauti.
Mashtaka hayo ni pamoja na kujifanya maofisa wenye mamlaka ya kutoa ajira, kinyume na kifungu namba 369, kifungu kidogo cha kwanza cha kanuni ya adhabu sura namba 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.
Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Beartha Richard, imedaiwa na Mrakibu Msaidizi wa Polisi ACP Geoffrey Kalugendo, ambaye pia ni Mkuu wa Operesheni wa Jeshi Wilaya ya Morogoro, kuwa washtakiwa hao 14 kati ya 15 waliokamatwa wanadaiwa, April Mosi, mwaka huu, majira ya alasiri, huko Kihonda, Azimio walijifanya maofisa wenye mamlaka ya kazi.
Wengine ni Elinuru Mollel (28), Erick Francis (22), Baraka Ally (21), David Joshua (22), Erick Onesmo (21),Anitha Elirehema (22), Donald Edward (22) na Dickson Akyoo (23), kwa pamoja wanadaiwa waliwakusabya vijana 48 kutoka sehemu mbalimbali nchini na kujipatia Pesa huku wakijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Hakimu Beatha aliahirisha shauri hilo hadi April 10, mwaka huu.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED