Mtambo (Bulldozer) huo unaomilikiwa na kampuni ya Uchimbaji madini ya dhahabu ya Bucreef umeparamia nyumba na kujeruhi watano na uharibifu wa nyumba tatu katika Kitongoji cha Isangiro,Kata ya Rwamgasa wilayani Geita mkono Geita.
Akizungumzia tukio hilo lililotokea Aprili 3,2025,Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba amesema dereva wa mtambo huo aliruka na kuuacha userereke umbali wa kilomita moja na kusababisha madhara.
Kiongozi huyo ambaye alifika eneo la tukio amesema dereva aliyekuwa akiuendesha alibainika kuiba mafuta na alipojua anafuatiliwa aliamua kuuacha kisha kukimbia kusikojulikana.
Kwa mujibu wa Komba, uchunguzi unaonesha mwendeshaji wa mtambo huo mtambo alijihususha na wizi wa mafuta na kwamba alikua na watu wawili baada ya watu wa mgodi kujua kuna wizi alianza kuondoka na alipogundua anafuatiliwa aliruka.
"Usiku wa saa nane mtambo huo uliparamia nyumba za wannachi wakiwa wamelala na kuvunja kuta na kwamba kupona kwa watu hao ilikuwa muujiza wa Mungu,"amesema.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED