SHIRIKISHO la michezo ya Pentathlon Tanzania (PMT) limeshiriki utaratibu wa kufanya usafii katika Fukwe za Dengu jijini Dar es Salaam kwa sababu mchezo huo unahitakiwa kufanyika sehemu safi.
Akizungumza na wanamichezo na washiriki waliokutana kwenye fukwe hizo kwa ajili ya kushiriki kufanya usafi Mkurugenzi wa Ufundi wa mbio za vikwazo, Joshua Kayombo amesema utaratibu huo umezinduliwa jana Aprili 05/2025 na utakuwa endelevu.
Kayombo amesema mchezo wa mbio za vikwazo unatakiwa kufanyika maeneo safi na salama na eneo la fukwe nalo ni miongoni mwa maeneo ya kufanyika michezo hiyo hivyo ni lazima yawekwe katika hali ya usafi.
"Michezo ya Mbizo za vikwazo huzingatia mambo mengi na miongoni ni sehemu safi na salama kwa mshiriki. Fukwe tutakazotumia kwa michezo hiyo lazima tuhakikishe ziko katika hali hiyo," amesema Kayombo.
Amesisitiza kwamba michezo ni afya kwa kila binadamu hivyo ni jambo la kuzingatiwa ili kuepuka maradhi yasiyo ambukiza.
Kwa mujibu wa Kayombo PMT kwa mwezi wote wa nne itafanya mchezo wa mbio za vikwazo katika eneo la Fukwe za Dengu kuanzia wiki ya pili ya tatu na ya nne kwa siku za Jumamosi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED