LIGI ya Taifa ya mpira wa wavu inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Julai 26 mwaka huu, kwenye viwanja vya Mwembe Yanga, Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la mpira wa wavu Tanzania, TVF, Shukuru Ally aliiambia Nipashe kwamba, Ligi hiyo itashirikisha timu 23 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara, ambapo kati ya hizo za Wanaume 14 na Wanawake 9.
Alisema lengo la Ligi hiyo ni kuuendeleza mchezo huo pamoja na kukukuza vipaji vya vijana.
Aliitaja mikoa ilithibitisha kushirki ni Mtwara, Ruvuma, Dodoma, Kigoma, Iringa, Morogoro, Arusha, Pwani pamoja na wenyeji Dar es Salaam.
"Maandalizi kuelekea kwenye Ligi hiyo yanaendelea vizuri, kila timu inaendelea kufanya mazoezi ili kuhakikisha inafanya vema,” alisema Ally.
Alisema kupitia Ligi hiyo vijana watapata fursa ya kujitangaza pamoja na kupata ajira kupitia mchezo huo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED