Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan amesema safari ya Watanzania kufanya shughuli za maendeleo bila kutegemea mikopo mikubwa inaanza ndani miaka mitano ijayo.
Dk. Samia ameeleza hayo leo Jumamosi wakati akizungumza na wananchi wa Dakawa wilayani Mvomero katika mwendelezo wa ziara ya kampeni za kusaka kura katika Uchaguzi Mkuu 2025 utakaofanyika Oktoba 29.
Ameto ahadi hiyo, akijrejea maandiko ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayoeleza kuwa ifikapo mwaka huo, Tanzania itakuwa yenye kipato cha kati cha ngazi ya juu na hakuna Mtanzania atakayelia na huduma za afya na elimu.
“Ifakapo mwaka 2050, Dira ya Taifa ya Maendeleo imeanisha kuwa hakuna atakayekosa huduma ya maji bora wala umeme wa kufanyika shughuli zake. Hii ndio Tanzania tunayoitaka. Tunaitaka Tanzania ambayo uchumi wake utasimama na kujitegemea.
“Tunaitaka Tanzania ambayo tutaishi na tutafanya shughuli zetu bila kuwepo na mikopo mikubwa, hii ndio Tanzania tunayoitaka ifakapo 2050 na safari yake inaanza ndani ya miaka mitano ijayo,”amesema Dk. Samia.
Ili kufanikisha suala hilo, Dkt Samia ambaye ni Rais wa Tanzania amewaomba wananchi wa Morogoro na Watanzania kwa ujumla kuipigia kura kwa wingi kukichagua Chama Cha Mapinduzi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED