Mgombea urais Chama Cha Mapinduzi (CCM) Samia Suluhu Hassan, ameomba ridhaa ya Watanzania kukichagua CCM kwa miaka mingine mitano ijayo akiwaeleza kwamba, chama hicho kina historia nzuri ya utekelezaji wa wanayoahidi.
Akizungumza leo na wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika eneo la Dakawa, wilayani Mvomero, mkoani humo, mgombea huyo wa urais amesema serikali imetekeleza Ilani ya Uchaguzi iliyopita kwa mafanikio makubwa.
“Kwa sababu CCM kina historia ya utekelezaji na bila shaka kuna kazi nzuri imefanyika kupitia ilani ya Uchaguzi 2020/25. “Ninataka niwaambie Chama Cha Mapinduzi na serikali yake imeendeleza ilani iliyopita. Mafaniko ya miaka minne iliyopita baadhi niliyataja juzi (Agosti 28) nikizindua kampeni zetu Dar es Salaam.
“Lakini wabunge kila maeneo nchini wanazungumzia mafanikio ya ilani. Hapa Mvomero mgombea wenu wa ubunge, Sara Msafiri, ameyaeleza,” amesema.
Mgombea urais Samia amewapongeza wana Mvomero kupitia sekta ya kilimo kwa kukuza na kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula pamoja na ya biashara.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED