Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Mariamu Ditopile, leo Agosti 26, 2025, amechukua fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Kondoa Mjini kupitia chama hicho.
Shughuli hiyo imefanyika katika Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo, ambapo wanachama wa CCM na wananchi walijitokeza kwa wingi kumpa sapoti.
Katika hatua nyingine, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa, Othuman Omary Duga, ametangaza kuwa chama chake hakitasimamisha mgombea katika Jimbo la Kondoa Mjini, ili kumpa nafasi Mariamu Ditopile.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED