Mashahidi 55 na vielelezo 54 vinatarajiwa kutumika Mahakama Kuu katika kesi ya mauaji bila kukusudia , yaliyosababishwa na kuporomoka kwa jengo la ghorofa Kariakoo,Dar es Salaam mwaka 2024.
Hayo yamesemwa na Wakili wa Serikili, Christopher Olembelle akisaidiana na Neema Kibodya, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Geoffrey Mhini, ambapo kesi hiyo rasmi imekabidhiwa Mahakama Kuu ya Tanzania kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji na mashahidi.
Katika shauri hilo baada ya washtakiwa wawili kuachiwa na DPP , wanaoendelea na mashtaka ni Leondela Mdete(49), Soster Nziku(55), Aloyce Sangawe(59)na Stephen Nziku(28) wote ni wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.
Aidha katika kesi hiyo, washitakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo Novemba 16, 2024 Mtaa wa Mchikichi na Kongo, Kariakoo ,jijini Dar es Salaam. Ilidaiwa kwamba, washitakiwa hao kwa pamoja walishindwa kutimiza majukumu yao na kusababisha vifo vya watu 31 ambao ni Said Juma, Hussein Njou, Prosper Mwasanjobe, Shadrack Mshingo, Godfrey Sanga, Neema Sanga, Elizabeth Mbaruku, Hilary Minja, Abdul Sululu, na Chatherine Mbilinyi.
Wengine ni Elton Ndyamkama, Mariam Kapekekepe, Elizabeth Kapekele, Hadija Simba, Frank Maziku, Rashid Yusuf, Ally Omary, Ajuae Iyambilo, Mary Lema, Khatolo Juma, Sabas Swai, Pascal Ndungulu, Brighette Mbembele, Ashery Sanga, Venance Aman, Linus Hasara, Issa Bakari, Lulu Sanga, Happnees Malya na Brown Kabovera
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED