MIAKA 28 baada ya kifo chake Bintinfalme Diana, bado anashikilia mioyo ya watu kote duniani. Akitajwa kuacha alama ya huruma umaarufu na kitamaduni, isiyofutika.
Katika maisha yake mafupi sana duniani, Diana alikuwa mwanamke maarufu zaidi na aliyepigwa picha zaidi, kuliko mwingine duniani. Kwa mtiririko wa watu maarufu duniani kupigwa picha nyingi.
Kwenye orodha kwa mujibu wa mtandao wa PhotoWhoa, wa kwanza ni Taylor Swift, akifuatiwa Bintimfalme Diana, Barack Obama, Kim Kardashian, Mfalme Charles III, Margot Robbie, Beyoncé, Donald Trump, Queen Camilla, Lionel Messi na Michael Jackson.
Diana, alifariki dunia Agosti, 31, mwaka 1997. Takribani miaka 28 baada ya kifo chake cha ghafla kutokana na ajali ya gari mjini Paris, Ufaransa, mwaka, dunia bado inavutiwa sana naye.
Wote watatu, Diana, Dodi Fayed na dereva, waliokumo kwenye gari iliyopata ajali eneo la ‘Pont de l'Alma tunnel’, walifariki dunia.
Mwandishi wa kitabu ‘Dianaworld: An Obsession’, Edward White, amemwelezea Bintimfalme Diana, kupitia mahojiano ya ‘zoom’ huko mtandaoni. Ndio msingi wa makala hii.
Kitabu kimechapishwa Aprili 29, 2025, kimefanya uchambuzi, baada ya kifo cha Diana. Kimechunguza jinsi alivyokuwa na athari isiyofutika kwenye tamaduni maarufu.
Tangu kifo cha bintimfalme huyo ni takribani miongo mitatu, tangu kifo chake akiwa na miaka 36.
Mwandishi, White, anazingatia watu aliowaona kujitambulisha kwa Diana, ikiwa ni pamoja na watu wanaofanana naye, wanaotafuta fursa na mashabiki wake wakubwa.
VIWANDA, BIASHARA ISIYO NA KIWANGO
Bintimfalme Diana, aliunganishwana bishara na wengine kunufaika, bidhaa zote ziliuzwa kwa sababu ya mvuto wake, akionekana amevaa wengine waliiga na kuzitafuta kwa bei yeyote.
Kuanzia vitabu, mavazi kama sweta maarufu ya ‘black sheep’ kutoka kampuni ya Warm & Wonderful, hadi bidhaa za ajabu zaidi kama mavazi ya ndani ya joto yalipata umaarufu, baada ya Diana kukiri kuyapenda kuyavaa wakati wa baridi.
Anasema Diana aliwahi kuhusishwa na kuokoa sekta ya kofia nchini Uingereza.
VIWANGO VYA JUU MAISHA, HARUSI NA MAZISHI
Inaelezwa kiwango cha juu cha Diana kilikuwa mara mbili duniani. Unaweza kuiita thmani hiyo ‘Dianamania’ ikimaanisha ‘thamani’ kutoka neno la kiarabu.
Julai 29, mwaka 1981, Diana Spencer (Bintimfalme), aliolewa na Prince Charles (sasa Mfalme Charles III) katika Kanisa la St. Paul, London, Uingereza.
Kadhalika, historia kubwa ilikuwa kwenye mazishi yake. Diana alizikwa Septemba 6, mwaka 1997, baada ya kifo chake Agosti 31, 1997.
Mwandishi huyu White, anasema, ‘mzuka wa harusi’ ulikuwa wa juu kwa ndoto Diana, ingawa baada ya kifo mazishi ilikuwa kitu tofauti kabisa, kwa viwango.
WIKI YA AJABU BAADA YA KIFO
Mwandishi White, anamweleza Diana akikumbuka wiki ile kati ya kifo cha Diana, huko Paris na mazishi yake London, kama kipindi kilichozua mijadala mikubwa kuhusu utambulisho wa kitaifa na mustakabali wa Waingereza.
Anasema katika kipindi hicho, Diana alivuka mipaka ya utu wa kawaida na kuwa ishara ya kitamaduni na mhusika wa kihistoria.
MASHADA YA MAUA, HISIA ZA TAIFA
Harufu isiyo kifani iliyotokana na mashada yasiyo na mwisho yenye maua yaliyoachwa nje ya jumba la kifalme ‘Kensington Palace’, ilikuwa ikihisiwa kutoka mbali, kama vile manukato ya mwilini.
Polisi walilazimika kuondoa maua yaliyooza, ili kuepuka matatizo ya kiafya.
Maua hayo ni mfano wa jinsi dunia, ilivyoguswa na hisia za watu.
HADITHI YA KIFALME, MVUTO WA KIPEKEE
Diana pia, ana hadithi za kifalme, hasa ya malkia au binti wa kifalme. Zimevutia watu kote duniani zaidi ya hadithi za wafalme na malkia.
Mfano wa mke wa Mwanamfalme William, kisasa ni Kate Middleton, mkwe wa Diana.
Anasema maisha ya kifalme kwa wanawake yana mchanganyiko wa mvuto na giza kubwa. Mara chache sana kuna ‘princess’ mpya anayepatikana.
MUDA MUAFAKA NA TEKNOLOJIA
Diana, aliibuka wakati teknolojia na vyombo vya habari vilipokuwa vikieneza habari na picha haraka zaidi. Magazeti ya rangi, vipindi vya runinga na nyaraka maalum.
Alikuwa ‘consumerist princess’ alikula migahawa maarufu kama McDonald’s. Alilia hadharani, aligusa watu bila glavu, kwa vyombo kila kitu kilikuwa ni habari kubwa kwao.
Alikuwa wa kipekee, mwenye huruma, lakini pia mara nyingine hakuona matokeo ya matendo yake.
KUVUNJA TARATIBU ZA KIFAMILIA
Diana, alivunja desturi za kifalme, akamsisitiza mwanawe William (akiwa na miezi tisa) asafiri nao (familia) hadi Australia mwaka 1983, kinyume na utaratibu wa kifalme.
Umaarufu wake ulikuwa kama wa nyota wa muziki kuliko wa kifalme.
MKUTANO WA MAAJABU HUKO
Renae Plant, mwanzilishi wa Makumbusho ya Bintimfalme Daina (‘The Princess Diana Museum), alimwona Diana kwa mara ya kwanza mwaka 1983, akiwa na umri wa miaka 12.
Diana alidondosha kinyago cha ‘platypus’ karibu naye, na mlinzi alimwambia huyo msichana…“Huenda amekudondoshea wewe….” Msichana huyo alikiokota.”
Tukio hilo lilimchochea Plant kuwa shabiki mkubwa wa Diana na baadaye aliamua kuanzisha makumbusho ya vitu vyake, ikiwamo alichokiokota.
MKUTANO WA PILI NA SHAUKU
Plant, alimwona tena Diana mwaka 1988, akiwa na umri wa miaka 18.
Wakati huu alimshika mkono na kuhisi ‘uwapo wa ajabu’ wa bintimfalme’.
Baada ya hapo, Plant alianza kukusanya nguo na vitu binafsi vya Diana, ili kuhifadhi urithi wake.
Kabla ya kufungua makumbusho hayo ambayo, Plant anavyosema kwa fahari, ni yasiyo ya faida mwaka 2014, alipata baraka zote kutoka kwa Prince William na Prince Harry, watoto wa Diana.
“Sikuzingatia kuanzisha kitu chochote kuhusu mama yao bila kuwajulisha, ni nini ningeanza kufanya?” anasema.
Plant, sasa, miaka 11 tangu kuanzishwa kwa makumbusho hayo anasema: “Nahisi kama bado tunaanza tu”.
MAKUMBUSHO YA KIDIJITALI
Makumbusho ya Diana, ina zaidi ya mavazi 100 ya Diana, vitu vya utotoni, mikanda ya muziki wa beatles, begi la Versace, pete za urafiki na barua.
Vitu vingine 14 vilitolewa kwa siri na mtu asiyejulikana, ili viwe sehemu ya makumbusho.
Miongoni mwa vitu maarufu ni rekodi ya Elton John yenye ‘Candle in the Wind’, wimbo aliouimba upya kwenye mazishi ya Diana mwaka 1997.
CHANGAMOTO ZA MABINTI WAFALME
Bintimfalme Diana, pamoja na mke wa mwanawe, Meghan Markle, hata kuolewa katika familia ya kifalme akiwa na umri wa miaka 36 ni changamoto.
Diana alikuwa karibu nusu ya umri wa Meghan, akiwa na miaka 20 tu. Wakati mtu anapojiunga na familia ya kifalme, pengo kati ya nafsi yako ya umma. Nafsi yako binafsi hupotea kwa kiasi kikubwa, anasema mwandishi White.
“Ni kweli kuolewa katika familia ya kifalme ni ngumu hata kama mume wako anakupenda kwa dhati. Ni lazima iwe changamoto zaidi wakati si hivyo.
Alikuwa na hitaji kubwa sana la upendo na kutiliwa mkazo na uthibitisho,” anasema White. “Lakini nadhani mwishowe alitafuta hayo katika sehemu zisizo sahihi, kama wanavyosema.
Diana, alikuwa na tabia mchanganyiko wa ajabu wa unyenyekevu, aibu na ujasiri hadi kiwango cha hatari.
“Na jambo hilo, hata baada ya kuandika kitabu, linanifanya niwe mgumu kuelewa jinsi alivyoweza kufanya haya yote yafanye kazi pamoja katika tabia moja.”
“Na zawadi kamili kwa wahariri wa magazeti. Na waliandika kuhusu yeye na walimchukua picha kila kitu kiliongeza umaarufu wake. Kila mtu, kwa namna fulani, ameguswa na yeye,” anasema White.
“Alikuwa karibu kabisa mtu wa kwanza kupokea matibabu makali ya paparazi, inamaanisha kwamba kuna hifadhi kubwa ya njia ambazo maisha yake yalichukuliwa picha. Hata baada ya kupata ajali.
“Jambo jingine linaloendelea ni kwamba kuna hadithi nyingi ambazo bado hazijamalizika na Diana. Mambo mengi ambayo watu hawajui, kwa sababu familia ya kifalme bado inafanya kazi kwa siri kubwa.
“Kutakuwa na kufichuliwa miaka 20 au 30 ijayo kuhusu maisha yake na kutakuwa na nafasi kwa vizazi vijavyo kuchukua na itakuwa kitu kingine.
Nadhani hadithi yake inamaanisha kitu tofauti kwa watu sasa, kitu kinachotofautiana sana kwa vijana Wa sasa (Gen Z), kuliko kilivyokuwa kwa vijana wa miaka ya 1980.”
Diana, bado anaendelea kuwapo katika maisha na midomo ya watoto wake Prince William na Prince Harry. Mvuto wa kitamaduni kwa Diana, hauonekani kuisha hivi karibuni.
“Hadithi ya maisha yake ilikuwa ya ajabu sana, tunaweza kumchunguza ni ya ajabu sana kiasi kwamba nina uhakika kuwa katika miongo michache ijayo, kutakuwa na toleo jipya la Diana, litakalovutia watu,” anasema White.
CHANZO: Forbes
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED