Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga, Oktoba 20, 2025, aliongoza maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali kufanya doria ya magari, miguu na mbwa wa polisi katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Akizungumza mara baada ya doria hiyo, Kamanda Kuzaga alisema kuwa hali ya usalama mkoani humo ni shwari na kwamba katika maeneo yote waliyopita, wananchi waliendelea na shughuli zao katika hali ya amani na utulivu.
Aliongeza kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limejipanga kikamilifu kuhakikisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao wakati wa kipindi chote cha uchaguzi.
“Natoa wito kwa wananchi wote kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29, 2025 bila hofu yoyote, kwani Jeshi la Polisi lipo kazini kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani,” alisema Kamanda Kuzaga.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED