Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, anaendelea kuchanja mbuga kunadi sera za chama hicho kwa Watanzania ili kumpa ridhaa kuongoza nchi, na asubuhi hii anatarajiwa kuunguruma Dakawa na baadae kuelekea Kilosa, Gairo na Kibaigwa.
Ikiwa ni siku ya tatu tangu kuanza kwa ziara yake ya kampeni CCM, Samia kwa muda huu wa asubuhi atanadi sera kwa wananchi wa Dakawa na baadae kuelekea Kilosa.Jana, baada ya kuwasili mkoani humo alifanya mikutano miwili, Ngerengere na baadaye jioni alifanya mkutano mkubwa uwanja wa Mkwawa, Morogoro.
Kwa mujibu wa ratiba ya leo, baada ya mikutano hiyo leo, ataelekea jijini Dodoma kwa mwendelezo wa ziara. Kampeni za CCM ilizinduliwa Agosti 28, 2025, katika viwanja vya Tanganyika Parkers Kawe, Dar es Salaam, maeneo yote aliyokanyaga maelfu ya wananchi wameitika kusikiliza sera, ili kuwawezesha Oktoba 29, 2025, kupiga kura na kuchagua viongozi wawatakao.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED