TUME ya Taifa ya Umwagiliaji inatarajia kujenga uzio na bwawa jipya katika shamba la umwagiliaji Dakawa, mkoani Morogoro. Hatua hiyo inalenga kulinda miundombinu, kuongeza tija ya kilimo na kuhakikisha wakulima wanapata maji ya uhakika kwa msimu wote.
Meneja wa Tume hiyo mkoani Morogoro, Mhandisi Juma Matanga, amesema mradi huo utasaidia pia kupunguza migogoro baina ya wakulima na wafugaji kutokana na mifugo kuharibu mazao na skimu za umwagiliaji.
Naye Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Tume hiyo, Maria Itembe, amesema Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imewekeza fedha nyingi katika miradi ya umwagiliaji kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa chakula cha kutosha na cha kuuza nje ya nchi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED