Chakula kilichochacha kinapoingia katika orodha afya bora nyumbani

By Tuntule Swebe , Nipashe
Published at 03:05 PM Oct 16 2025
 Lishe ikichakachuliwa.
Picha; Mtandao
Lishe ikichakachuliwa.

KATIKA jamii kumezoeleleka dhana kwamba chakula kinapochacha, huwa kimeharibika. Hata hivyo, kurejea uhalisia wake si kwa vyakula vyote. Kuna upande wa manufaa kwa baadhi ya vyakula.

Hapo ndipo mwandishi wa makala hii katika jitihada za kupata picha sahihi akamuona mtaalamu na Ofisa Lishe, anayetumikia hospitali kubwa jijini Dar er Salaam, Abubakar Mzee, akitoe ufafanuzi wa kitaalamu.

Msomi huyo anatofautisha chakula cha kuchacha kwamba ni kile kilichoharibika, huku kilichochachushwa ni kilichofanyiwa mabadiliko ya uhalisia wake.

Mtaalamu Mzee, anafafanua kwamba michakato ya uchachushaji imekuwapo kwa vizazi katika utamaduni mbalimbali.

Mtazamo wake ni kurahisisha uhifadhi na maisha bora ya chakula. Umaarufu wa vyakula vilivyochacha, huwa unaanzia katika ladha, hadi thamani yake ya lishe na manufaa yake kiafya.

Safari ya uchachushaji chakula na vinywaji mathalan maziwa, ni mchakato unaohusisha ukuaji wa viumbe vilivyodhibitiwa na shughuli zake kama vile kubadilisha sukari na wanga katika chakula, kuwa pombe au tindikali.

Hiyo ni kama vile katika uhifadhi wa asili wa mchakato huo, unaoboresha ladha na muundo wa chakula mfano siki inavyotengenezwa.

FAIDA YA KUCHACHUSHA 

Mtaalamu wa Lishe- Abubakary Mzee, anatamka kuwapo faida za kiafya za chakula kilichochachushwa, kwamba kinaboresha ‘uyeyushaji chakula kilichochacha’ kukipunguzwa matatizo ya usagaji chakula, ikirejesha uwiano wa bakteria rafiki kwenye utumbo.

Mtaalamu Mzee, anasema baadhi huongeza kinga na uchunguzi umeonyesha kuwa katika afya ya utumbo, ikimpa mtu uwezo zaidi wa mtu wa kupambana kukabili maambukizi.

Pia, anataja kuwa chakula kilichochachushwa huwa kina Vitamini C, madini chuma na zinki zinazosaidia kuimarisha kinga na kupona haraka mgonjwa, kutokana na maambukizi.

Eneo lingine mtaalamu Mzee analitaja kwamba, ni katika suala la kuwa na afya ya moyo katika chakula kilichochacha, hupunguza shinikizo la damu na kupunguza ‘lehemu’ (cholesterol) inayoweza kusababisha magonjwa ya moyo kwa mtu.

Kuna suala la kupungua uzito - uchunguzi umeonyesha kuwa aina fulani za ‘probiotic’ zinaweza kusaidia kupoteza uzito na kupambana na mafuta ya tumbo.

Pia, anataja kurahisisha chakula kwa urahisi kilichochashwa tayari kimevunjwa na bakteria, hivyo kuwa rahisi kusagika.

Anasema kuna watu kimaumbile hawana matatizo ya kuyeyusha bidhaa za maziwa zilizochacha, hivyo mchakato huo unabaki kuwa rahisi.

Kwa mujibu wa mtaalamu huyo, kuna suala la shida ya afya ya akili kwamba:  Sehemu ya lishe pale inapochachushwa, huhusishwa na kupunguza dalili za wasiwasi na huzuni.

Vyakula hivyo vilivyochachushwa vinajumuisha lishe, mtaalamu Abubakary Mzee akitamka mfano wa mlo maziwa na mtindi, yamemegawanyika katia makundi.

Hapo kunatajwa kuwapo yale yaliyofanyiwa mchakato kabla ya uchachushaji, vikiwekewa bakteria rafiki wa uchachushaji.

Akizungumza maziwa ambayo hayajafanyiwa uchachushaji na kuyahifadhi, kwa kawaida yanaweza kuleta madhara kama vile homa za matumbo, ndivyo ilivyo kwenye vyakula vyote.

MIFANO YA MLO

Maziwa ya mtindi, hifadhi yake huanzia kuyachemsha na baadaye kuweka bakteria rafiki wa uchachushaji.

Hatua ya kuchemsha kinga  magonjwa ya matumbo na faida ya chakula ikisaidia mfumo wa lishe na umeng’eshaji chakula.

Ofisa Lishe Jamii huyo Mzee, anatamka kwamba watu inatakiwa watu wazingatia kitaalamu jinsi ya kuchachusha chakula kwa kutumia hatua rafiki, zitakazosaidia kuimarisha afya ya utumbo, kwa kuingiza bakteria rafiki kwa mfumo wa afya.

Mtindi inatengenezwa kwa kuchachusha maziwa na bakteria wa n tindikali aina ya lactic’. Uchunguzi unaonyesha kuwa ni chakula kijachosaidia kupunguza shinikizo la damumu na kuboresha msongamano wa madini ya mfupa mwilini kwa watu wazima wazee.

Pia anaitaja Tempeh Tempeh; hiyo imetengenezwa kutoka kwenye soya iliyopikwa na kuchachushwa. Ni chakula cha jadi nchini Indonesia, mbadala wa nyama. 

Mlo huo untajwa kuwa chanzo kizuri cha protini na ina kinga kwa ajili ya afya ya mlaji.

 Kombucha; ni aina ya chai inayopendwa na watu wenye uwezo mkubwa, ikitokana na kuchachushwa na bakteria, sukari na chai. Inafaa katika matibabu ya ugonjwa wa ‘bowel’, wenye hasira, hata kuhara, pia ikihusishwa na faida katika afya ya akili.

Kimchi - Ni kachumbari iliyochacha yenye viungo, maarufu katika vyakula vya Kikorea. Kimchi hutayarishwa kwa kuchachusha mboga kama kabichi na tango.

Inasaidia kudhibiti sukari katika damu, kupunguza uvimbe na kulinda afya ya moyo.

Sauerkrautl; hiyo imetengenezwa kwa kusagwa kabichi iliyochachushwa na bakteria katika tindikali. Inaaminika kuwa asili yake ni China, lakini sasa imegauka kitoweo maarufu katika utamaduni tofauti. 

Inachukuliwa kuwa ya manufaa kwa afya ya utumbo, afya ya ubongo, kupoteza uzito na kinga.

Natto;chakula cha jadi cha kijapani kilichotengenezwa kutoka soya iliyochachushwa. Huwa ina nyuzi, vitamini K2 na mengine hata kudhibiti shinikizo la damu na athari za lehemu. Pia ni muhimu, kukabili matibabu ya magonjwa ya kuambukiza ya bakteria.