Manara, Zaylissa ndiyo basi!

By Vitus Audax , Nipashe
Published at 07:34 PM Apr 10 2025
Manara, Zaylissa ndiyo basi!
Picha: Mtandao
Manara, Zaylissa ndiyo basi!

Kama ni umfuatiliaji wa mitandao ya kijamii hasa Instagram kuanzia Aprili 9, 2025 basi utakuwa na maswali ya je ndoa Haji Manara pamoja na muigizaji wa tamthiria ya Jua Kali na mwanamitindo Zaylissa iliyovuma mitandaoni ndiyo basi au vipi.

Ndoa ya wawili hao ambayo hivi karibuni ilitimiza mwaka mmoja imeonekana kuingia doa baada ya wao kuanza kurushiana maneno mitandaoni huku Zaylissa akionekana kuomba talaka kwa muda mrefu bila mafanikio kwa kile anachodai kuwa ni kushindwa kuvumilia tabia za Manara.

Alichokiandika Zaylissa


“Mtu Mzima ovyo ww, m…….zi mkubwa Imetosha Sasa nimechoka kupretend...Sasa Acha tuvuane nguo Kama ulivyozoea. Mtoto wa dada Angu amekuja kukaa likizo kwa mapenzi na muda wake wa kuondoka ulivyofika ulimzuia!

Kumbe ulikuwa unamtongoza shame on you Ulikuwa na kazi ya kumshika shika m…..wa binti mdogo wa under 18! Sasa round hii umechezea pabaya Umezoea kulala ma house girl Sasa ukaona uhamie kwa binti yangu loh.

Unamtumia mtoto vi 50k vyako Akiwa shule ili umlaghai Kwa taarifa yako tuna ushahidi wote! Na driver wako pia anajua kila kitu na tumeambiwa na hatutakukalia kimya Kila nikiomba talaka yangu hutaki kunipa jina…zi we Unagombana na Mimi unamwambia kijana wako arecord Kisha unaongea vya uongo! Unantishia kupeleka kwa mange ili unidhalilishe...Sasa round hii sicheki na kima Kama ushazoea kudhalilishana Ntakupa unachostahili.” - Zaylissa


 Hata hivyo Haji Manara alijibu kwa kuandika

“Umekuja hata nguo huna ya kuvaa Leo unasema jogoo wangu hapandi mtungi!

Unawanyima wanangu chakula.


Bora watu waseme naoa sana ,Wacha aende tu..”

“Mama yangu na Baba yangu na Watoto wangu wapo juu ya kila kitu duniani kasoro Mungu tu.,,

Heri nisemwe naoa sana lakini Mwanangu hadi kunyimwa chakula nnachokihangaikia baba yake kwa jasho jingi,,sikubali abadan,,

Mtanisamehe Waja wa Manani 🙏🙏
AENDE TU”

Baada ya kile kinachoelezwa kuwa Zaylissa amepokea talaka yake kutoka kwa Manara, aliandika katika mtandao wake kuwa.

“Thanking God for guiding me out of darkness and into the light. It was the hardest decision, but today, I stand stronger and more determined than ever. I’m excited and blessed to be working with incredible brands as a brand influencer, a path I’m embracing with open arms. Remember, healing is possible, and your past does not define your future. Keep moving forward.”


Akimaanisha kuwa "Namshukuru Mungu kwa kuniongoza kutoka gizani na kuniingiza kwenye nuru. Ulikuwa uamuzi mgumu zaidi, lakini leo, ninasimama imara na nimedhamiria zaidi kuliko hapo awali. Ninafuraha na kubarikiwa kufanya kazi na chapa za ajabu kama mshawishi wa chapa, njia ninayoikumbatia kwa mikono miwili. Kumbuka, uponyaji unawezekana, na maisha yako ya nyuma hayaainishi maisha yako ya baadaye. Endelea kusonga mbele."

Hata hivyo alipotafutwa Manara kujibia suala la kutoa talaka kwa Zaylissa alijibu kuwa kwa sasa hana la kuzungumza tofauti na chapisho lake aliloliweka awali mtandaoni ambalo mwisho lilieleza kuwa ‘AENDE TU’.

“No comment post niliyoweka inatosha”….Manara.


Dulla Makabila aingia studio

Katika mtandao wake wa Instagram msanii wa mziki wa singeli Dulla Makabila ambeye pia alikuwa Mume wa Zaylissa amechapisha akiwa studio.

Katika chapisho lake Makabila akifuatiwa na mdundo wa mziki wa uzuni nyuma ya picha mjongeo ameuliza mashabiki wake kuwa wanahitaji wimbo muda gani.

"MNATAKA SAA NGAPI ?"