Real Madrid wamepata nguvu kubwa baada ya kipa Thibaut Courtois kuteuliwa katika kikosi kitakachosafiri kwa ajili ya mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Arsenal Jumanne.
Courtois ambaye amekosa mechi tatu zilizopita akiwa na Real Madrid kutokana na jeraha, huku ripoti nchini Hispania zikisema amekuwa akipata maumivu yaliyosababishwa na uvimbe kwenye sehemu ya nyuma ya goti lake.
Andriy Lunin amekuwa akisimama goli kwaajili ya timu hiyo wakati ambao Mbelgiji huyo hayupo, lakini alikosa kichapo siku ya Jumamosi dhidi ya Valencia kutokana na jeraha la mguu.
Hata hivyo Real Madrid walilazimishwa kucheza na Fran Gonzalez, ambaye ana umri wa miaka 19 pekee, golini hivyo kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Valencia.
Lunin hatakuwa fiti kwa wakati kumenyana na Arsenal, hata hivyo Courtois ameitwa kwenye kikosi cha Real Madrid kitakachosafiri kwenda London Jumatatu asubuhi.
Madrid walifanya mazoezi nchini Uhispania siku ya Jumapili na Courtois alishiriki katika mazoaezi hayo.
Carlo Ancleotti hana wachezaji kadhaa wa kikosi cha kwanza, hata hivyo, na ni pamoja na Aurelien Tchouameni - ambaye amesimamishwa kwa mechi ya kwanza ya robo fainali Jumanne huko Arsenal.
Dani Carvajal na Eder Militao wamekuwa nje tangu mwishoni mwa mwaka jana kutokana na majeraha ya goti na bado hawapo. Dani Ceballos na Ferland Mendy pia wameachwa kwenye kikosi kitakachosafiri kwenda Arsenal kutokana na majeraha.
Ceballos, ambaye alitumia misimu miwili kwa mkopo Arsenal kutoka 2019 hadi 2021, alifanya mazoezi ya ndani siku ya Jumapili kabla ya kujiunga na kundi zima kwa kipindi fulani.
Ceballos alikuwa mmoja wa wachezaji wanne wa Real Madrid ambao walihatarisha kupigwa marufuku na UEFA kwa pambano la Jumanne kwenye Uwanja wa Emirates.
UEFA ilianzisha uchunguzi kuhusu sherehe za Antonio Rudiger, Kylian Mbappe, Vinicius Junior na Ceballos baada ya ushindi wa Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid katika raundi ya mwisho.
Hakuna hatua za kinidhamu zilizoletwa dhidi ya Vinicius, huku Mbappe na Rudiger wote wakipigwa faini na kupewa adhabu ya kufungiwa mechi moja. Ceballos alipigwa faini.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED