Mshambuliaji wa Bayern Munich, Harry Kane amesema mchezo dhidi ya Inter Milan utakuwa ni mgumu lakini timu hiyo inaweza kuishinda timu yoyote kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya (UCL).
Mwingereza huyo amebainisha hayo saa kadhaa kuelekea mechi ya mkondo wa kwanza ya robo fainali inayotarajiwa kuchezwa siku ya jumanne wakianzia katika uwanja wao wa nyumbani.
Inter na Bayern ni kati ya vilabu vilivyopambwa zaidi barani Ulaya, ukizungumza kihistoria.
Vinara hao wa sasa wa ligi katika Serie A na Bundesliga mtawalia ni miongoni mwa timu zilizoingia kwenye kampeni ya sasa kati ya zinazopendekezwa kuinua kombe la Ligi ya Mabingwa.
Wakati huohuo, Inter na Bayern wanakabiliana na majeraha kadhaa kabla ya mechi hiyo ya mkondo huo wa kwanza ambako Bayern haswa wako katika hali ya mzozo kabla ya pambano hilo.
Kane Mshambuliaji wa zamani wa Tottenham Hotspur mwenye umri wa miaka 31 ndiye mfungaji bora wa Bavarians msimu huu.
Ameweka wazi kwamba lengo lao ni kufanikiwa na ili kufikia hilo, wanahitaji kila mtu.
Kane amesema kuhusu majeruhi ya Bayern kwa sasa kwamba watatumika zaidi wachezaji ambao hawachezi mara nyingi, "Lakini hakuna visingizio. Kila timu inahusika na majeraha na kutokuwepo."
Mshambulizi wa Bayern Harry Kane alisema wazi kwamba "tumeweza kudhibiti hali hizi vyema msimu mzima sasa si wakati wa kuacha," aliongeza mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza.
Harry Kane alikiri kwamba "ana ndoto ya kushinda Ligi ya Mabingwa kwa maisha yake yote kuifanya katika uwanja wetu wa nyumbani kungeifanya kuwa ya kipekee zaidi," ameongeza mchezaji huyo.
"Itabidi tuwe tayari, tukijua kwamba katika siku zetu, tunaweza kumshinda mtu yeyote."
Mwingereza huyo alisema kwamba "Tayari tumeonyesha hivyo."
"Lakini hapa litakuwa suala la kuwa thabiti katika mechi ya kwanza na ya pili. Kisha tutaona tunachoweza kupata, tukikumbuka kwamba sote tuna motisha ya ziada."
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED