Mchezaji wa zamani wa timu ya Arsenal Philippe Senderos amesema mchenzaji mwenzake wa zamani ambaye kwa sasa ni kocha wa timu hiyo Mikel Arteta endapo atatumia nondo zake atashinda mikondo miwili ya michezo baina yake na Real Madrid.
“Niliishinda Real Madrid nikiwa na Arsenal…hii ndio sababu mchezaji mwenzangu wa zamani Mikel Arteta anaweza kufanya vivyo hivyo,” amesema Senderos.
Timu ya Arsenal inajiandaa kwa robo fainali ya mikondo miwili dhidi ya Real Madrid katika Ligi ya Mabingwa huku watabili mbalimbali wakionesha kuwa timu hiyo haitokuwa na uwezo wa kuiondosha Madrid katika kinyang’anyio hicho.
Licha ya utabili huo, Senderos anaamini kuwa kikosi cha Mikel Arteta kinaweza kuiga washika bunduki wake na kuwashangaza Real Madrid wakielekea fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Akirejea rekodi za nyuma katika msimu wa 2005-06, Senderos anasema haukuwa na shauku zaidi dhidi ya wababe hao wa Uhispania.
Senderos ambaye alikuwa sehemu ya mabeki wanne walioongozwa na Arsene Wenger ambao hawakuruhusu bao lolote katika dakika 540 za soka la mtoano kabla ya Barcelona kuwazuia jijini Paris. Mbio ikianza kwa ushindi wa bao 1-0 ulioongozwa na Thierry Henry kwenye Uwanja wa Bernabeu, huku Juventus na Villarreal pia wakikumbana na kichapo.
“Timu ya Arteta haiwezi kufikia rekodi hiyo ya ulinzi, lakini iliifunga PSV Eindhoven 9-3 katika hatua ya 16 bora na itawakaribisha mabingwa wa sasa wa Ligi ya Mabingwa kwenye Uwanja wa Emirates siku ya Jumanne.
Senderos, ambaye alicheza kwa muda mfupi na meneja wa Arsenal huko Everton, anaona uwezekano mkubwa kwa timu hiyo kuchukua ushindi endapo mambo muhimu yatazingatiwa na kocha pamoja na wachezaji ikiwemo kuimarisha ulinzi na kutokuruhusu goli.
"Ninakumbuka mchezo huo sana kwa sababu baba yangu ni Mhispania na ni shabiki wa Real Madrid, kwa hivyo kwangu ilikuwa kama kuishi moja ya ndoto zangu kucheza dhidi ya Real Madrid huko Bernabeu," Senderos amesema.
"Sasa mechi ya kwanza ni nyumbani, lakini tunajiandaa kwa mchezo kama huu, shinikizo la mchezo huu, wakati huo ningesema matarajio kutoka kwetu ni kujaribu kufanya bora dhidi ya Galacticos.
"Shinikizo lilikuwa zaidi kwa Real Madrid kufanya kweli na tulikuwa nje kidogo, naweza kusema. Tulijiandaa kama tulivyofanya kwa kila mechi ya Uropa, tukiingia humo tukijua tulikuwa vizuri, tukijua kwamba tunaweza kuwapiga, na ilifanyika vyema!"
Senderos anaeleza kutambua changamoto ya kukabiliana na safu ya mbele ya timu ya Uhispania inayotisha kupitia Kylian Mbappe aliyejiunga na mabingwa hao wa Uropa msimu uliopita, lakini sio rahisi kama kumzuia nyota huyo wa zamani wa Paris Saint-Germain.
"Mkomeshe, halafu lazima umsimamishe Vinicius na kisha Rodrygo!" anaongeza. "Wao [Madrid] wana wachezaji wa ajabu, na itabidi kuwa na mbinu ya pamoja.
"Arsenal italazimika kukaa vizuri sana, kukuza winga, na hii itahitaji kazi kubwa kutoka kwa viungo, kutoka kwa mabeki wa pembeni, kuhakikisha nafasi si kubwa."
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED