KATIKA jamii na maisha ya kibaolojia, hoja ya nafasi ya nguvu za kiume inachukua nafasi kubwa.
Ni aina ya mijadala inayokaa zaidi ngazi ya chini, kuliko ghorofani. Lakini kwa kuwa inabeba maisha ya watu, tafsiri yake inaangukia uzito mkubwa.
Kwa wahusika wakuu wanaume wengi wamekuwa wakipata shida katika kutimiza haja zao, vilevile kwa wanaopokea ambao ni wenza wao katika uhusiano.
Walio wengi wanapokumbwa na tatizo hilo, hukimbilia kwenye suluhisho la siri wanazama katika dawa za asili wakiamini ina majibu kamili.
Pia, wapo wanaojisogeza hospitalini bila kujua kilichojificha nyuma ya pazia na vijana ndio zaidi wahusika zaidi, pasipo kujua mara nyingine wanajizamisha zaidi katika hatari.
Wengi wanachosahau, kabla ya kupiga hatua, wanapaswa kuanza na darasa linalowaelewesha kasoro iliko, pia namna ya kuikabili.
Hapo ndipo penye elimu ya jumla katika jamii inatakiwa, ikijibu maswali kama, je wajua mtu akipata maboga, tende, ndizi za kuiva, parachichi, pia maziwa mtindi anakuwa ameshaanza safari ya kujikimu?
Ni hatua bora ya mtu kuanza nayo, hata kabla ya kuanza safari kwenda kumwona daktari akihisi shida bado haijaondoka.
Mbali na kuwa tiba, pia kiafya ni safari bora kimwili iwe kwa mwanaume au mwanamke.
Kudodosa zaidi, uthubutu wangu unaangukia kumdadisi mwenye taaluma hiyo ya tiba, akijibu hoja hizo,
Mtaalamu Dk.Wiiliam Mgisha wa Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI), anafafanua kuwa kitabibu na kiafya, kuwapo mbegu za maboga, tende, ndizi, parachichi na maziwa vina uwezo wa kuongeza nguvu za kiume.
Hiyo ni kwa sababu vyakula hivyo, vina vitu umuhimu wa kukimu hicho kinacholalamikiwa.
Mbegu za maboga anazitaja kuwa na madini ya potasiamu, calcium na zinki.
Anaendelea kuwa, katika tende kuna sukari, pia madini zinki, huku parachichi inamwongeza mlaji mafuta na vitamini.
Hivyo, mtu yeyote akipata chakula bora anakuwa na uwezo mzuri na hasa zaidi kwa wanaume kujikimu na afya hiyo ambayo ina sura ya starehe.
Nikaamua kuendeleza undani wa darasa langu na nikigonga hodi aliko Daktari Azizi Butogo wa Hospitali ya Manispaa Ubungo, Dar es Salaam.
Naye akaziunga mkono mlo wa; parachichi, mbegu za maboga, tende, ndizi, maziwa mtindi kwamba zina uwezo wa kuongeza nguvu za kiume.
Pia, hapo akataja zinaendana na kuweka sukari sawa na mtu kupata uwezo wa kufanya kazi.
Nafasi yake, wenye magonjwa wanaopata tatizo la nguvu za kiume, kuhisi yenye mjumuiko ulioungwa mkono na madaktari, ina maana kubwa sana kuwekeza katika afya.
Mtaalam huyo akasema, licha ya kwamba hakuna utafiti wa jumla, lakini katika ukanda wa mtu mmoja mmoja, bado ina nguvu zake.
Nami kwa elimu niliyopata ninamaanisha kwamba, fursa ya mlo bora nayo ni sehemu ya tiba kwa mengi, zaidi ya tuliyoyaona hapa. Mathalan, juisi hiyo katika ujumla wake ni tiba kubwa wengi wetu tunaweza kufanyia kazi
Napenda kutumia ushuhuda wa mkazi wa Tegeta kwa Ndevu aitwaye....(jina tunalo), Dar es Salaam, anayetamka kuwa na miaka saba ya ndoa na mkewe, alishawahi kupatwa na tatizo hilo la nguvu za kiume kwa miaka mitatu.
Anasema baada ya kuzunguka mitaani kutafuta suluhisho, matumizi ya mahitaji yaliyoorodheshwa akayataja kumpa majibu ya kukwama kwake katika nguvu za kiume, katika uwezo hata hamu yake.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED