WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken amehimiza uchaguzi mkuu wa Senegal ambao umeahirishwa, ufanyike haraka iwezekanavyo katika tarehe iliyokuwa imepangwa au kama sio hivyo basi ufanyike haraka bila kucheleweshwa.
DW imeripoti kuwa, Blinken ameonesha wasiwasi kuhusu kucheleweshwa kwa uchaguzi huo baada ya kuwasiliana kwa njia ya simu na Rais Macky Sall wa Senegal.
Marekani kupitia Wizara yake ya Mambo ya Nje, imesema ina wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya Taifa hilo la Afrika Magharibi ambalo Jana February 13 lilizuia mawasiliano ya intaneti na kupiga marufuku maandamano.
Katika hatua inayofanana na hiyo, Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema haki ya Wasenegali kuandamana kwa amani ni lazima iheshimiwe.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED