Siri kuhusu wingi wa aina mpya ya nyumba maalum za kuishi watalii au wageni (AirBnB na Home Stay) katika mikoa ya Kaskazini ya Arusha na Kilimanjaro, imefichuka.
Ni mfumo wa kibiashara unaovutia watalii wanaokodi nyuma kwa siku kadhaa lakini tofauti yake na lodge ni moja, mgeni anakutana na vitu tofauti, ambapo AirBnB au Home Stay huwa na vitu vyote vya nyumbani, mfano jiko, sebule yenye viti na meza, runinga na kitanda.
Akizungumzia usalama wa malazi hayo ya wageni katika mahojiano maalum, Mrakibu wa Polisi (SP), Waziri Tenga, ambaye ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Utalii na Diplomasia-Mkoa wa Arusha, amesema AirBnB na Home Stay hazitofautiani, isipokuwa ni majina yanayotumika kuongeza mvuto.
"Aina hii ya malazi imeshamiri zaidi kaskazini mwa Tanzania, na ni kitu kinachomfanya mtalii ajihisi kama yuko nyumbani, tofauti na lodge ambako huwa na chumba cha kulala pekee.
"AirBnB na Home Stay, ni malazi ambayo wageni wengi wanayapenda, kwa hiyo mgeni anapata hadi location na dereva taxi au bodaboda anayefika mahali hapo. Utaona zinavyoongeza mnyororo wa thamani na ukuzaji uchumi wa kaya au familia zinazotoa nyumba zao kwa ajili ya uwekezaji wa malazi.
...Kwa hiyo flycatcher’s huwezi kuona anapata wapi tena mgeni.AirBnB/Home Stay zinasajiliwa. Kuna utaratibu wa kusajili kupitia mamlaka husika lakini pia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wanasajili. Kuna mamlaka ya masuala ya utalii na hata Halmashauri, ukienda ukasajili nyumba yako, wanakuja wanakagua wanakupa leseni ya biashara."
Kwa mujibu wa Tenga, AirBnB/Home Stay, ni fursa kubwa kiuchumi, akisisitiza ukiona mahali zinashamiri ujue eneo hilo ni salama.
Katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, wamiliki wenye Home Stay na AirBnB, wako zaidi ya 178, ambapo Kituo cha Polisi Utalii na Diplomasia, kimewaunganisha kundi moja, kwa ajili ya kutoa taarifa za uhalifu na watu wanaowatilia mashaka.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED