Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni" msemo huu umejidhihilisha katika familia ya Mzee Futakamba baada ya familia hiyo kuamua kufanya sherehe ya ndoa licha ya bibi harusi mtarajiwa kukataa.
Watu wengi wamezoea kufanya sherehe ya ndoa kwaajili ya kufurahia ndoa yao kufungwa iwe kanisani au mskitini lakini kwa familia ya Futakamba wakazi wa Makanyagio Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi jambo hilo limekuwa tofauti .
Familia hiyo imejikuta katika hali ya mshangao baada ya ndoa ya kijana wao iliyokuwa ifungwe Julai 26, 2024 kuingia dosari siku tatu kabla ya ndoa baada ya bibi harusi mtarajiwa na familia yake kwenda kanisani kuzuia kufungwa kwa ndoa hiyo.
Edward Futakamba ambaye alikuwa bwana harusi anasema anamshukuru Mungu kwa yote yaliotokea kwani kupata na kukosa yote ni sehemu ya maisha.
"Kwakweli tumepata hasara watu walikua wameandaa kila kitu,gauni na mapambo yote ya bibi harusi yamegharimu thamani ya laki tano (500,000) gauni bado lipo nyumbani hadi sasahivi" alisema
Justina Futakamba ni mzazi wa aliyekuwa bwana harusi mtarajiwa anasema "Sina mengi ya kueleza kitu nachoshukuru ni sherehe imefana, jinsi mnavyoona huyu ni kijana wangu wa kwanza na hichi kitu hakijawahi kutokea kwenye familia.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED