Viongozi wa dini mkoani Shinyanga wametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ifikapo Oktoba 29 mwaka huu, ili kutimiza haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi bora watakaowaletea maendeleo kuanzia ngazi ya mitaa.
Viongozi hao, kwa umoja wao, wameazimia kuunga mkono jitihada za serikali katika kuhamasisha wananchi kushiriki uchaguzi kwa amani, utulivu na umoja wa kitaifa.
TAMKO
Wakizungumza kwa pamoja, viongozi hao wamesisitiza kuwa kila Mtanzania ana wajibu wa kutunza amani, kwani amani ndiyo tunu na msingi wa maendeleo ya taifa.
Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Lazaro Nyalandu, amewaomba viongozi wa dini, machifu na wazee wa kimila kuendelea kuliombea taifa hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi, ili nchi iendelee kuwa na umoja na utulivu.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Mboni Mhita amewahakikishia wananchi kuwa siku ya kupiga kura itakuwa salama, na akawataka kujitokeza kwa wingi kutekeleza wajibu wao wa kiraia bila hofu.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED